JUMAZA KUAZISHA CHUO KWAAJILI YA WANANDOA.

Na Mwandishi Wetu,  Zanzibar

JUMUIYA ya Maimamu Zanzibar (JUMAZA) itaazisha chuo maalum Visiwani zanzibar  kwa ajili ya wana ndoa ili kuepuka kuongezeka talaka na vitendo vya ukatili wa kijinsi.


Akizungumza na mwandishi wa blog hii, Katibu Mtendaji wa Jumuiya hiyo Visiwani hapa  Muhidin Zubeir Muhidin,  alieleza kuwa chuo hicho ni kwa wazanzibari wanaotaka kuingia au waliomo ndani ya ndoa ili kujenga familia zenye maadili bora.

Alieleza kuwa chuo hicho kiko hatua za mwisho mtaala umo kwenye hatua za kupitiwa na Afisi ya kadhi Mkuu ili kipata baraka za serikali.

“Jengo tayari tunalo ambalo linataka kufanyiwa marekebisho kidogo ambayo yatagharimu kiasi cha milioni 10.(10,000,000)” alieleza Ustadhi Muhidini.

Alisema kuwa Chuo  kitasaidia sana kupunguza matatizo ya wanandoa na kuleta kutengamaa vyema kwa  familia na kitasaidia sana kuondoa udhalilishaji  wa kijinsia.

“Mfano talaka ni halali lakini vipi inatolewa, na Jee ikishatolewa
watoto watahudumiwa na nani, hayo yote tutayasomesha kwa kina ili kupunguza au kuwa na talaka zenye kufuata taratibu na siyo mtu kuamka akatoa talaka” alieleza Muhidini.

Zanzibar imekuwa ikikumbwa na mrundiko wa talaka kwana na ndoa hasa vijana wanao owa na kuolewa siku hizi za karibuni.

Alieleza kuwa pia chuo hicho kitasaidia kupunguza ama kuondoa kabisa tatizo la ukatili wa Kijinsi.

Licha ya Udogo wake Zanzibar inakadiriwa na kutolewa talaka ama kwa kupitia majumbani au kwa Mahakama ya Kadhi zaidi ya 2000 kwa mwaka.



Comments

Popular posts from this blog

SERIKALI YAREJESHA KAMBI TANO ZA JKT ZILIZOKUWA ZIMESITISHA MAFUNZO YA JESHI.

BELENG’ANYI, MBUNIFU MWENYE MALENGO YA KUTENGENEZA MGODI WA KUFUA UMEME.

WAKULIMA WA ZAO LA VITUNGUU IRINGA WATELEKEZA MASHAMBA.