MAKINDA NIDHAMU YA KAZI NA KUJALI MUDA NDIO KILICHOWAFANYA KOREA KUSINI KUFANIKIWA.
Na Mwandishi Wetu.
SPIKA wa Bunge wa Jamhuri ya Muungo wa Tanzania Mstaafu,
Anne Makinda, amesema nidhamu ya kazi na kujali muda ndio kilichowafanya Korea Kusini
kufanikiwa kimaendeleo.
Hayo aliyasema jana, wakati akizindua Taasisi isiyokuwa
ya Kiserikali ya Chingu Kota Centre inayojishughurisha na kutangaza utamaduni
wa Korea nchini Tanzania.
Makinda, alisema
nchi ya Korea Kusini ilikuwa nchi masikini kama sisi kwa kipindi cha miaka ya
nyuma ila nchi hiyo kwa sasa ipo juu kwenye masuala ya kiuchumi ukilinganisha
na nchi yetu ambayo ina madini na rasilimali nyingi.
“Korea Kusini suala kuchelewa chelewa kama sisi hawana, wao wanajali sana muda na
hakuna kitu mali kama muda, muda ni mali kuliko kitu chochote,”alisema na
kuongeza kuwa
“Wanafanya kazi kwa nidhamu hata mwendo wao ni wa nidhamu
tofauti na sisi tunatembea muda wote kama tumechoka,”
Naye, Mwanzilishi na Rais wa Chingu Kota Centre, Andrew Dyson Bukuku alisema taasisi hiyo itakuwa kituo kitakachoshughurikia vyuo Vikuu kutoka nje ya Tanzania na ndani ya Tanzania kwaajili ya kuwaelimisha watu utamaduni wa korea.
“Kwa mfano Korea ukikuta bomba limepasuka, wanapiga ngoma watu wote watatoka kwaajili ya kuja kusaidiana kulitengeneza ila kwa sisi hapa ukikuta hivyo utaacha na kusema maji si ya Dawasco hayo,”alisema
Kwa upande wake Project Manager Nasibu Koko, alisema Chingu Kota Centre iliazishwa kwa lengo la kuwaweka wadau wa maendeleo na tamaduni za Asia na Tanzania.
“Na katika nchi za Asia tumeaza na Korea Kusini kwani uchumi wake ulikuwa sawa sawa na nchi za Afrika lakini leo hii nchi hiyo ni moja kati ya nchi zenye uchumi mkubwa dunia,”
Aidha Mkutano huo wa siku tatu ulihudhuriwa na wanafunzi kutoa Chuo cha Amity Haryana kilichopo India, Profesa Kumari Mansi na Kunal Anand pamoja na Dokta Sabine Burghart kutoka Chuo cha Vienna.
Picha ya Pamoja na Spika wa Bunge Mstaafu Anne Makinda baada ya kufungua mkutano huo jana jijini Dar es Salaam.
Rais na Mwanzilishi wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Chingu Kota, Andrew Bukuku katika picha ya pamoja na wageni wake wa ndani na kutoka Korea Kusini na China.
Spika Mstaafu, Anne Makinda (wa pili kulia) akimsikiliza Profesa, Geofrey Calimag kutoka Korea akizungumzawakati wa Mkutano wa kujadili utamaduni wa Korea Kusini na nchi zingine za Asia uliowahusisha wanafunzi wa vyuo vikuu Jijini Dar ea Salaam mei 25, 2017, kulia ni Rais na Mwanzilishi wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Chingu Kota, Andrew Bukuku na kushoto ni Mweka hazina wa Taasisi hiyo, Pamela Bukuku
Rais na Mwanzilishi wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Chingu Kota, Andrew Bukuku (kulia) akizungumza wakati wa Mkutano wa kujadili utamaduni wa Korea Kusini na nchi zingine za Asia uliowahusisha wanafunzi wa vyuo vikuu Jijini Dar ea Salaam mei 25, 2017. kushoto ni Profesa, Geofrey Calimag kutoka Korea na Spika Mstaafu, Anne Makinda.(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA).
Comments
Post a Comment