RAIS DKT MAGUFULI APOKEA KWA MASIKITIKO VIFO VYA WANAFUNZI 32, VILIVYOTOKEA KWA AJALI ARUSHA.
KAMANDA WA POLISI ARUSHA
Na Mwandishi Wetu.
WANAFUNZI 32, walimu wawili na derava mmoja wa Shule Lucky Vincent Nursery & Primary iliyopo Arusha, wamefariki dunia baada ya Coastar waliyokuwa wakisafira
kupinduka eneo la mlima Rock Wilaya ya Karatu.
Akizungumzia ajali hiyo leo , Kamanda wa Polisi, mkoa wa Arusha, Charles
Mkumbo amesema Costar hiyo yenye Namba za usajili T. 781 iliyokuwa imebeba
abiria zaidi ya 38 iliyokuwa ikitokea Arusha imepinduka na kusababisha vifo vya watu 35 huku watano wakiwa mahututi.
Kamanda Mkumbo, alisema katika ajali hiyo wanafunzi 32 na watu
wazima watatu wakiwamo walimu wawili na
dereva mmoja wamefariki dunia katika ajari
hiyo.
Pia alisema bado wanaendelea kuchunguza chanzo cha ajali hiyo
pia, huku akisema hali za mahututi sio nzuri.
Muonekano wa gari aina ya Coastar iliyokuwa imepakia wanafunzi wa Shule ya Lucky Vincent Nursery & Primary iliyopo Mkoani Arusha.
Baadhi ya Miili ya wanafunzi hao iliyotolewa eneo la Rhotia Marera baada ya basi hilo kuacha njia na kutumbukia korongoni.
Baadhi ya wananchi walioenda kushuhudia ajali hiyo wakishuhudia uokoaji wa maiti hizo.
Comments
Post a Comment