Peter Akaro BINADAMU anazaliwa na ubunifu au mazingira anayokuliwa yanaweza kumfanya kuwa hivyo. Makala ya leo yatazungumzia maisha ya mbunifu Ntibanga Beleng’anyi ambaye anatengeneza mashine za kukamulia juisi ya miwa na kuunda magari. Pengine vitu hivi si vigeni katika mazingira yetu, ila kilichopelekea makala haya kuandikwa, ni namna Beleng’anyi alivyoweza kutengeneza vitu hivi bila kusomea sehemu yoyote. Ndiyo hakusoma, Baada ya kumaliza Shule ya Msingi Ng’wang’iwita iliyopo Bariadi Shinyanga, mwaka 2005 aliamua kuja Dar es Salaam kwa ajili ya kazi za kibunifu kwa sababu upatinaji wa vifaa ni rahisi, vitu alivyofanikiwa kutengeneza ni kama. Hii ni mashine ya kutengenezea juisi ambayo inatembea umbali wa kilo mita 400. MASHINE YA JUISI. Mashine ya kukamua juisi ya miwa ambayo kaitengeneza yeye ina utofauti katika vitu viwili ukilinganisha ni zile zilizozoeleka, kwanza mtumiaji ana uwezo wa kuitembeza hadi umbali wa meta 400 kutokana ina matairi. Pi...
Comments
Post a Comment