Zefrin Lubuva, afungua blog ya mtaa, S MTAA OYSTERBAY.BLOGSPOT.COM
Na Enles Mbegalo
MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa Oysterbay, Zefrin
Lubuva, amefungua blog ya mtaa wake kwaajili ya kutumia mambo mbalimbali ya
kimaendeleo kwenye mtaa wake.
Akizungumza na mwandishi wa blog hii jijini Dar es
Salaam leo, Lubuva, alisema ufunguzi wa blog hiyo ni moja ya ahadi zake ambazo
alizitoa kwa wakazi hao wakati wa
uchaguzi.
“Mtaa wangu ulikuwa hauna blog na nimetekeleza hili
ili liweze kutusaidia kwaajili ya kupeana taarifa mbalimbali za maendeleo zinazofanyika kwenye
mtaa wetu,”alisema Lubuva
Lubuva, alisema wadau mbalimbali walio kwenye mtaa
wetu wamekuwa wakichangia huduma mbalimbali kwaajili ya maendeleo ya mtaa na blog hii itasaidia wananchi
kuwafahamu wadau hao zaidi na huduma ambazo wamekuwa wakizitoa kwenye mtaa.
“Blog yetu ya mtaa wa Oysterbay nataka iwe ya mfano
katika mitaa yote ya Dar es Salaam,”alisema
Comments
Post a Comment