WATU WA NANE WAVAMIA MKUTANO WA CUF NA KUJERUHI.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
BAADHI ya waandishi wa habari na wanachama wa Cufu
wajeruhiwa baada ya watu wanane, waliokuwa wamevalia ninja na kuvamia mkutano
wa wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF), mabibo jijini Dar es Salaam.
Vurugu hizo
zimetokea leo, wakati wanachama wa CUF
walipokuwa kwenye mkutano huo na waandishi wa habari katika Hoteli ya Viva
jijini Dar Es Salaam.
Vurugi hizo zilizua taharuki kubwa kwa waandishi wa
habari na wakazi wa eneo hilo ambapo walifanikiwa kumkamata mmoja wa watuhumiwa
hao na kumkata mguu wa upande wa kulia.
Hata hivyo baadhi ya mashuhuda wanasema watu
wasiojulikana walifika katika eneo hilo wakiwa wamefunika nyuso zao na vitambaa
huku wakitumia silaha za jadi.
Hata hivyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi
Kinondoni, Suzan Kaganda, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na taarifa zaidi
atatujuza baada ya kufika eneo la tukio.
Mmoja wa watuhumiwa akipambana na wananchi baada ya kukamatwa eneo la tukio jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa watuhumiwa waliovamia mkutano huo akiwa chini ya ulinzi baada ya kukatwa mguu wake wa kulia na wananchi.
Comments
Post a Comment