DIWANI URIO AWA MIONGONI MWA WALEZI WA KITUO CHA WATOTO YATIMA AMANI ORPHANAGE.
Na Enles Mbegalo
DIWANI wa Kata ya Kunduchi jijini Dar es Salaam,
Michael Urio,amejitolea kuwa miongoni mwa wazazi watakao kuwa walezi wa kituo
cha kulelea watoto yatima cha Amani Orphanage, kilichopo Bagamoyo Mkoa wa
Pwani.
Aidha, Diwani Urio alijitolea wakati alipokuwa mgeni rasmi katika uchangishaji wa
harambee kwaajili ya kuchangisha fedha za kusaidia katika kutatua baadhi ya
changamoto zilizopo kwenye kituo hicho.
“Na mimi nitakuwa miongoni mwa wazazi watakao lea
kituo hiki na shida yangu itakuwa shida yao, kama nilivyo mzazi wa familia
yangu naomba niwe mzazi wa kituo hiki,”alisema Urio na kuongeza kuwa
“Mkurugenzi usisite kunishirikisha kitu chochote iwe
chakula, mavazi, malazi nitawasaidia kwa nilichonacho na nitawasaidia kuomba
kwa wadau mbalimbali kwaajili ya watoto hawa,”
Hata hivyo pamoja na ulezi huo Diwani Urio aliahidi
kutoa Sh. Milioni moja pamoja kusaidia kufikisha umeme kwenye eneo hilo
kutokana na kutokuwa na umeme.
Pia Diwani Urio ameahidi kusaidia ujenzi wa madarasa
ya Shule kwenye eneo la kituo hicho kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali.
Hata hivyo Mkurugenzi wa Kituo hicho alimshukuru Diwani Urio kwa kuweza kuchangisha zaidi ya Sh. Milioni Sita kwenye harambee hiyo ambazo zitatumika katika kuweka Solar kwenye eneo hilo na kutatua baadhi ya changamoto za kwenye kituo hicho.
Diwani Urio akiwa Pamoja na Mkurgenzi wa Kituo hicho akimpeleka sehemu ya kukaa mara baada ya kufika kwenye kituo hicho.
Diwani Urio akipiga makofu wakati wa uchangishaji wa harambee hiyo katika kituo hicho leo.
Diwani Urio aliyenyanyua mtoto akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wadau na watoto wanaolelewa kituo hicho .
Mkurugenzi wa Kituo hicho pamoja na Diwani Urio wakicheza wakati mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Christina Mbilinyi akitumbuiza kwenye hafla hiyo iliyofanyika kwenye kituo hicho.
Baadhi ya wada wa kituo hicho kutoa TEAMTEZZA na TEAMVW zinazohusika na ushindanishaji wa mbio za magari, kutoka Kunduchi jijini Dar es Salaam.
Melone Africa katika akiwa na baadhi ya watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho.
Baadhi ya wadau wakiwa wanaondoka kwenye kituo hicho baada ya hafla hiyo kumalizika.
Miongoni mwa wadau walioshiriki kwenye hafla hiyo leo wakiwa kwenye picha ya pamoja.
PICHA ZOTE NA MAISHA NI HABARI BLOG.
Comments
Post a Comment