Posts

Showing posts from May, 2017

DIWANI URIO, KUZINDUA KAMPENI YA WEZESHA MAMA NA MTOTO MPYA WA KUNDUCHI.

Image
Ungana na Diwani Kata ya Kunduchi  Michael Urio, katika Kampeni ya Wezesha Mama na Mtoto Mpya wa Kunduchi , yenye lengo la kuwezesha ujenzi wa wodi ya akina mama pamoja na chumba cha upasuaji katika Zahanati za Mtongani na Ununio ndani ya Kata ya Kunduchi. Uzinduzi wa Kampeni hii utahusisha ufanyaji wa usafi katika Zahanati ya Mtongani siku ya  Jumamosi tarehe 3/6/2017.         Karibuni Wote. Matukio mbalimbali ya Kampeni hii yatatolewa na MAISHA NI HABARI BLOG, siku ya jumamosi.

KICHAA WA YESU AJA NA WIMBO MPYA WA USINIACHE YESU.

Image
John Mgina maarufu kama Kichaa wa Yesu anakuja na wimbo mpya unaofanya vizuri USINIACHE YESU.   Ujio wa mwaka 2017 Albam inaitwa HAYA NI MAPITO TU. Mgina anapatikana kwa namba 0756 896976.

WABUNI INJINI ISIYOTEGEMEA MAFUTA KUJIENDESHA.

Image
 Shukuru Machupa na David Ng’unda wakiwa wameshikilia kifaa hicho. Peter Akaro KATIKA kupambana na kuhakikisha sayansi inaleta unafuu wa kimaisha, vijana wawili kutoka chuo cha st. Joseph Dar es Salaam wamefanikiwa kubuni kifaa (injini) walichokipa jina la ‘Green Energy Heat Exchanger’ kama nishati mbadala isiyoharibu mazingira. Ni David Ng’unda na Shukuru Machupa wanaeleza kuwa kifaa hiki ni aina ya injini ndogo yenye kutumia mfumo wa ubadilishaji wa joto la hewa au gesi ambayo hupatikana ndani ya silinda (heat exchanger). Joto hilo linaweza kutokana na chanzo chochote kama vile jua, moto, maji ya moto, au hewa ya moto kutoka kwenye mashine nyingine. Kifaa kinaweza kuunganishwa na mifumo mbalimbali ya kiutendaji katika kuzalisha nishati ya umeme, mifumo hii ni kama ule wa bio ges, mfumo wa kutumia mvuke, mifumo yote hii inatoa majibu chanya katika uwezeshaji wa mashine hii kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kutoa msukumo zaidi katika ufanyaji kazi wake. Hivyo

NBS IMEANZA MAANDALIZI YA UTAFITI WA MATUMIZI YA TUMBAKU KWA WATU WAZIMA NCHINI.

Image
  Mtaalam wa Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima, David Plotner (kushoto) kutoka shirika la CDC Marekani akijadiliana na maafisa wa TEHAMA wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Munir Mdee (katikati) na Abdullah Othman (kulia) wakati wa mafunzo ya awali ya utafiti huo yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima unatarajia kufanyika nchini mwezi Agosti, 2017.   Afisa TEHAMA kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Munir Mdee akitoa mafunzo ya kutumia Dodoso kwa njia ya tablet kwa washiriki wa mafunzo ya Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima wakati wa mafunzo ya awali ya utafiti huo yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.   Mratibu wa    Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima,Hellen Hillary (kushoto) kwa upande wa Tanzania Bara akijadiliana na mratibu wa utafiti huo kwa upande wa Tanzania Zanziar  , Nuru    Masoud (kulia) wakati wa mafunzo ya awali ya utafiti huo yaliyofanyika hivi karibuni jijin

WAIMBAJI WA INJILI WALIVYOSIFU NA KUABUDU LEO KATIKA KITUO CHA IBAADA CHA MCC.

Image
  Waimbaji wa Nyimbo za Injili Tanzania, Richard Mmari pamoja na mke wake Christina Seme wakiimba nyimbo katika ibaada ya leo ya kituo cha  Ibada cha Mliman City Worship Centre (MCC) , jijini Dar es Salaam .  Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Tanzania John Mgina maarufu kama Kichaa wa Yesu akiimba kwenye madhabahu ya MCC leo . Waumini wakiendelea kuimba katika kipindi cha sifa katika kituo cha ibaada cha MCC leo.   Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Tanzania, Dk. Isaya Msangi (MD), akiimba mbele ya madhabahu ya mlimani City, ambapo hufanyika ibaada kila siku ya jumapili kuanzia saa 8:00 hadi 11:00 kwenye ukumbi wa sinema uliopo ndani ya jengo la Mlimani City jijini Dar es Salaam, kituo hicho ambacho kimeanzishwa kwaajili ya kutoa huduma ya maombezi kwa madhehebu yote na hakuna kiingilio.   Waimbaji wa Nyimbo za Injili Tanzania, wakiongoza kipindi cha siafa leo, katika kituo cha ibaada cha MCC kushoto Christina Seme, katikati ni Jackline Skamwa na kulia ni Slivanus Mumba.

MAABARA SABA ZA UCHUNGUZI WA MAGONJWA YA BINADAMU MKOANI IRINGA ZAFUNGIWA.

Na Mwandishi Wetu, Iringa. BODI   ya Usajili na Usimamizi wa Maabara Nchini imezifungia maabara saba za uchunguzi wa magonjwa ya binadamu zilizopo katika Halmashauri mbalimbali mkoani Iringa kwa kukiuka taratibu za uendeshaji huduma hizo ikiwamo kutumia wataalamu wasio na sifa jambo linalokiuka sheria namba 10 ya uanzishwaji na uendeshaji wa maabara ya mwaka 1997. Akizungumza mjini Iringa jana Kaimu Mkaguzi wa Bodi hiyo, Ednanth Gareba alisema bodi hiyo imekagua maabara zaidi ya 40 na kubaini mapungufu makubwa kwenye maabara hizo ambapo asilimia 50 ya maabara zilizokaguliwa    zilikuwa hazijakidhi vigezo vya kutoa huduma hiyo. Gareba alisema kuwa wao kama serikali wanachohitaji ni huduma bora kwa watanzania wote na sio huduma, wanavyofungia maabara hizo wameona hakuna namna nyingine ya kufanya tofauti na kufunga kwa sababu hawana watalamu. Naye Ofisa Utawala Kituo cha Afya Nyololo, Diana Yesaya ,alisema baadhi ya wamiliki na wasimamizi wa vituo vya afya na maabara wana

CHAMA CHA SKAUTI TANZANIA KUADHIMISHA MIAKA 100 JULAI 21 HADI 28 MWAKA HUU.

Image
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar CHAMA cha Skauti Tanzania kinatarajia kuadhimisha miaka 100  ifikapo Tarehe 21 hadi 28 Julai  Mwaka huu  katika Kampasi ya Chuo Kikuu Makao Makuu Mjini Dodoma. Aidha Vijana wapatao 5,000 kutoka Wilaya zote za Tanzania Bara na Zanzibar pamoja na zaidi ya wageni 1,000 kutoka Nje ya Tanzania wanatarajiwa kushiriki maadhimisho hayo. Taarifa iliyotolewa jana kwenye vyombo vya habari  na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Othman Khamis Ame inasema kuwa Mkuu wa Skauti Tanzania, Mwatum Mahisa alieleza hayo alipokuwa  akiuongoza Ujumbe wa Viongozi  Tisa wa Chama hicho Bara na Zanzibar alipokuwa akitoa Taarifa hiyo kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar.  Mwatum, alisema vugu vugu la maadhimisho hayo limekuja kufuatia ziara ya Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania wa Awamu ya Nne Mizengo Peter Pinda alipofanya ziara ya kuhudhuria maadhimisho ya Skauti Nchini Uganda Mwaka 2016. Alisema kutokana na uzito

JUMAZA KUAZISHA CHUO KWAAJILI YA WANANDOA.

Na Mwandishi Wetu,   Zanzibar JUMUIYA ya Maimamu Zanzibar (JUMAZA) itaazisha chuo maalum Visiwani zanzibar  kwa ajili ya wana ndoa ili kuepuka kuongezeka talaka na vitendo vya ukatili wa kijinsi. Akizungumza na mwandishi wa blog hii, Katibu Mtendaji wa Jumuiya hiyo Visiwani hapa  Muhidin Zubeir Muhidin,  alieleza kuwa chuo hicho ni kwa  wazanzibari wanaotaka kuingia au waliomo ndani ya ndoa ili kujenga  familia zenye maadili bora. Alieleza kuwa chuo hicho kiko hatua za mwisho mtaala umo kwenye hatua za kupitiwa na Afisi ya kadhi Mkuu ili kipata baraka za serikali. “Jengo tayari tunalo ambalo linataka kufanyiwa marekebisho kidogo ambayo yatagharimu kiasi cha milioni 10.(10,000,000)” alieleza Ustadhi Muhidini. Alisema kuwa Chuo  kitasaidia sana kupunguza matatizo ya wanandoa na kuleta kutengamaa vyema kwa  familia na kitasaidia sana kuondoa udhalilishaji  wa kijinsia. “Mfano talaka ni halali lakini vipi inatolewa, na Jee ikishatolewa watoto watahudumiwa

MAKINDA NIDHAMU YA KAZI NA KUJALI MUDA NDIO KILICHOWAFANYA KOREA KUSINI KUFANIKIWA.

Image
Na Mwandishi Wetu. SPIKA wa Bunge wa Jamhuri ya Muungo wa Tanzania Mstaafu, Anne Makinda, amesema nidhamu ya kazi na kujali muda ndio kilichowafanya Korea Kusini kufanikiwa kimaendeleo. Hayo aliyasema jana, wakati akizindua Taasisi isiyokuwa ya Kiserikali ya Chingu Kota Centre inayojishughurisha na kutangaza utamaduni wa Korea nchini Tanzania. Makinda,  alisema nchi ya Korea Kusini ilikuwa nchi masikini kama sisi kwa kipindi cha miaka ya nyuma ila nchi hiyo kwa sasa ipo juu kwenye masuala ya kiuchumi ukilinganisha na nchi yetu ambayo ina madini na rasilimali nyingi. “Korea Kusini suala kuchelewa chelewa  kama sisi hawana, wao wanajali sana muda na hakuna kitu mali kama muda, muda ni mali kuliko kitu chochote,”alisema na kuongeza kuwa “Wanafanya kazi kwa nidhamu hata mwendo wao ni wa nidhamu tofauti na sisi tunatembea muda wote kama tumechoka,”   Naye, Mwanzilishi na Rais wa Chingu Kota Centre, Andrew Dyson Bukuku alisema taasisi hiyo itakuwa kituo kitakacho

FORMER SPEAKER OF THE NATIONAL ASSEMBLY MAKINDA HAS CHALLENGED THE TANZANIAN TO LEARN FROM SOUTH KOREAN CULTURE.

Image
By Correspondent. Former Speaker of the National Assembly Anna Makinda has challenged the Tanzanian to learn from South Korean culture of hard working and time management that accelerates economic development in South Korea. She made the remarks yesterday in Dar es Salaam in a conference to launch the  Korea and Tanzania friendship project 'CHINGU KOTA CENTRE' a project focusing on promoting South Korea Culture in Tanzania. Makinda said that Tanzania has a lot to learn from South Korea due to the fact it is one among the developed country in Asia Continent. Themed; “Building Connections and Strengthening Ties through Education” the conference is basically to link the higher learning students from Tanzania with the one from South Korea to acquire exposure and exchange academic issues. “Tanzania students will have time to learn from South Korea on various science courses basing on mechanical and civil engineering, but also will learn on how South Korea are ab