WATANZANIA WATAKIWA KUWA WAVUMILIVU NA SIO KUTAFUTA NJIA YA MKATO.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam WATANZANIA, wametakiwa kuwa wavumilivu kwa jambo lolote wanalolifanya na sio kutafuta njia za mkato kufikia malengo yao ambazo zitawafikisha pabaya. Wito huo umetolewa leo na Askofu Mkuu wa Dayosisi Kuu ya Dar es Salaam na Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania (KMUT), Emmaus Mwamakula, katika kituo cha Ibada cha Mliman City Worship Centre (MCC). “Watanzania tuwe wavumilivu na sio kutafuta njia za mikato kwenye maisha yetu kwani jambo lolote lile jema hufanywa kwa bidii na sio kutumia njia za mkato,”alisema na kuongeza “Tujifunza uvumilivu kama neo la leo lilivyosema, tuogope mambo ya mkato kwani mambo haya yatatupeleka mahali pasipo pazuri,” “Mfano katika nchi yetu siku hizi za karibuni Rais Dkt. John Pombe Magufuli alikabidhiwa Ripoti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) na kubaini mambo mbalimbali ikiwamo baadhi ya watumishi wa umma kugushi vyetu na walifany...