ZOEZI LA KUOROZESHA KAYA KWA AJILI YA UTAFITI WA MAPATO NA MATUMIZI KUANZA LEO
Meneja wa Takwimu za
Jamii na Watu Bi. Sylvia Meku akizungumza wakati wa mafunzo ya Wadadisi
watakaokwenda kuorozesha kaya mikoa yote kwa ajili ya maandalizi ya Utafiti wa
Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18. Zoezi hilo
la uorozeshaji kaya litafanyika kwa muda wa siku kumi na tano (15) kuanza leo Julai 11, 2017.
Baadhi
ya Wadadisi wakimsikiliza kwa makini Meneja wa Takwimu za Jamii na Watu Bi.
Sylvia Meku (hayupo Pichani) wakati wa mafunzo ya Wadadisi watakaokwenda
kuorozesha kaya mikoa yote kwa ajili ya maandalizi ya Utafiti wa Mapato na
Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18. Zoezi hilo la uorozeshaji
kaya litafanyika kwa muda wa siku kumi na tano (15) kuanza leo Julai 11, 2017.
Baadhi ya Wadadisi
wakiwa kwenye gari wakielekea Kata ya Mchikichini, Ilala na Kawe jijini Dar es
Salaam kufanya mazoezi ya kuorozesha kaya kwa vitendo kwa ajili ya maandalizi
ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka
2017/18. Zoezi hilo la uorozeshaji kaya litafanyika kwa muda wa siku kumi na
tano (15) kuanza leo Julai 11, 2017.
Baadhi ya Wadadisi
wakielekezwa namna ya kutumia ramani wakati wa kufanya mazoezi ya kuorozesha
kaya kwa vitendo na Mtalaam wa Ramani Jumanne Msuya wa Ofisi ya Taifa ya
Takwimu (katikati) kwa ajili ya maandalizi ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya
Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18. Zoezi hilo la uorozeshaji kaya
litafanyika kwa muda wa siku kumi na tano (15) kuanza leo, Julai 11, 2017.
(PICHA
ZOTE NA EMMANUEL GHULA)
Na Veronica Kazimoto, Dar es Salaam
WADADISI wa Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa
Mwaka 2017/18 wameaswa kuzingatia maadili ya kazi wakati wa zoezi la kuorozesha
kaya linalotarajia kuanza kesho ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya utafiti huo.
Akizungumza wakati wa
mafunzo ya siku mbili yaliyofanyika jijini Dar es Salaam kwa wadadisi hao,
Meneja wa Takwimu za Jamii na Watu, Sylvia Meku kutoka Ofisi ya Taifa ya
Takwimu amesema ili kufanikisha zoezi la uorodheshaji wa kaya, ni lazima
wadadisi hao wakazingatia maadili ya kazi pamoja na kufuata taratibu zote za Utumishi
wa Umma.
“Ofisi ya Taifa ya Takwimu
inawaagiza kwenda kwenye jamii kwa ajili ya kuorodhesha kaya zitakazofanyiwa
Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18.
Natumaini mtatii na kuheshimu maadili ya Utumishi wa Umma ili muweze kufanikisha
kazi hii kwa ufanisi,” amesema Slyvia Meku.
Alisema Zoezi la Uorodheshaji
wa Kaya litafanyika mikoa yote ya Tanzania Bara kwa takribani siku 15 kuanzia
leo Julai 11, 2017 na baadae kufuatiwa na utafiti wenyewe unaotarajia kuanza
mwezi Desemba, 2017.
Sylvia Meku alisema utafiti
huu unafanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha
na Mipango na baadhi ya Wadau wa Maendeleo kwa lengo la kuangalia kiwango cha
umasikini nchini.
Comments
Post a Comment