ZOEZI LA KUORODHESHA KAYA KWA AJILI YA UTAFITI WA MAPATO NA MATUMIZI LINAENDELEA KUFANYIKA NCHINI
Mdadisi
kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akihoji taarifa za kaya wakati wa zoezi
la kuorodhesha kaya kwa ajili ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi
Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 linaloendelea kufanyika nchini ikiwa ni
maandalizi ya utafiti huo unaotarajia kufanyika hivi karibuni.
Mdadisi
kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akihoji taarifa za kaya wakati wa zoezi
la kuorodhesha kaya kwa ajili ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi
Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 linaloendelea kufanyika nchini ikiwa ni
maandalizi ya utafiti huo unaotarajia kufanyika hivi karibuni.
Mdadisi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akiwaoneyesha
wasimamizi namna alivyojaza taarifa za kaya wakati wa zoezi la kuorodhesha kaya
kwa ajili ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa
Mwaka 2017/18 linaloendelea kufanyika nchini ikiwa ni maandalizi ya utafiti huo
unaotarajia kufanyika hivi karibuni.
(PICHA
ZOTE NA EMMANUEL GHULA).
Na Veronica Kazimoto, Dar es Salaam
ZOEZI la kuorodhesha kaya kwa ajili ya Utafiti wa
Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 linaendelea
nchi nzima ikiwa ni maandalizi ya utafiti huo unaotarajia kufanyika hivi
karibuni.
Akizungumzia zoezi hilo, Meneja wa Takwimu za
Jamii na Watu, Sylvia Meku wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu amesema mpaka sasa
mikoa kumi na tatu (13) imekamilisha zoezi hilo ambapo ni sawa na silimia 50.
“Zoezi la kuorodhesha kaya kwa ajili ya Utafiti
wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 linaendelea
vizuri na mpaka sasa wadadisi wamekamilisha kuorodhesha kaya katika mikoa 13,”
amesema Sylvia Meku.
Ameitaja mikoa iliyokamilisha zoezi la
uorodheshaji wa kaya kuwa ni pamoja na Dar es Salaam, Arusha, Manyara, Iringa,
Njombe na Morogoro. Mikoa mingine ni Mwanza, Tabora, Katavi, Mbeya, Mara,
Kagera na Lindi.
Zoezi la Uorodheshaji wa Kaya linafanyika mikoa
yote ya Tanzania Bara na linatarajia kumalizika mwishoni mwa mwezi Julai, 2017.
"Utafiti kama huu mara ya mwisho ulifanyika Mwaka 2011/12 ambao ulionesha
kuwa asilimia 28.2 ya Watanzania wanaishi chini ya mstari wa Umaskini wa mahitaji
ya Msing,"
Utafiti wa Mapato na Matumizi
ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 unafanywa na Ofisi ya Taifa ya
Takwimu kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango na baadhi ya Wadau wa
Maendeleo kwa lengo la kupata viashiria vya kupima hali ya umaskini nchini.
Comments
Post a Comment