CHAMA CHA MADEREVA “BAJAJI” KIMEIOMBA SERIKALI KUTOTOA LESENI KWA MADEREVA WASIO NA SIFA.
Mwenyekiti wa chama cha Maendeleo ya Madereva Pikipiki Matairi
Matatu Tanzania, Edward Mwenisongole akizungumza na madereva hao leo baada ya mgeni rasmi Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Ofisi ya Mkoa wa
Polisi Kinondoni, Samson J. Nguno, kuwasili katika mkutano huo.
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Ofisi ya Mkoa wa
Polisi Kinondoni, Samson J. Nguno, akisaini kitabu cha wageni baada ya kufika.
Wageni kutoka Kampuni ya Shinyanga Emporium na wauzaji wa pikipiki na bajaji aina Piagio, waliofika kwenye mkutano huo leo jijini Dar es Salaam kwaajili ya kutoa elimu ya fursa juu ya mikopo ya bajaji na pikipiki.
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Ofisi ya Mkoa wa
Polisi Kinondoni, Samson J. Nguno, akimkabidhi cheti mmoja wa madereva wa bajaji waliohitimu mafunzo hayo ya wiki mbili na kutunukiwa vyeti leo.
Madereva wa bajaji waliotunukiwa vyeti leo wakinyoosha mikono baada ya Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Ofisi ya Mkoa wa
Polisi Kinondoni, Samson J. Nguno, kuwataka kunyoosha mikono watu walioshiriki mafunzo hayo na ambao watatunukiwa vyeti hivyo.
Madereva wakishangilia baada ya Mwenyekiti wa chama hicho, Edward Mwenisongole kusema madereva ambao hawana sifa za udereva hawatapewa leseni.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Shinyanga
Emporium na wauzaji wa pikipiki na
bajaji aina Piagio, Herman Bernard, akizungumzia jinsi kampuni hiyo inavyotoa mikopo hiyo ya bajaji na pikipiki.
Madereva bajaji wakifuatilia ugawaji wa vyeti hivyo leo.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Shinyanga
Emporium na wauzaji wa pikipiki na
bajaji aina Piagio, Herman Bernard ,akionyesha moja ya bajaji ambazo zinakopeshwa na kampuni hiyo.
Madereva bajaji waliotunukiwa vyeti vya mafunzo ya udereva leo.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Shinyanga
Emporium na wauzaji wa pikipiki na
bajaji aina Piagio, Herman Bernard, akizungumza na mmoja wa madereva pikipiki ambaye alihitaji ufafanuzi juu ya mikopo inayotolewa na kampuni hiyo.
(PICHA ZOTE NA MAISHA NI HABARI).
Na Enles
Mbegalo
CHAMA cha Maendeleo ya Madereva Pikipiki Matairi
Matatu Tanzania kimeiomba serikali kutotoa leseni kwa madereva ambao hawana sifa za udereva ili kuepuka
ajari ambazo zinawaacha madereva vilema.
Ombi hilo limetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa chama hicho, Edward
Mwenisongole wakati akisoma risala kwa mgeni rasmi wakati wa tukio la kukabidhi
vyeti kwa madereva 110 waliohitimu mafunzo ya udereva.
“Tunapendekeza madereva wote ambao hawana sifa za
udereva wasipewe leseni na wale ambao wanaleseni lakini hawajapata mafunzo ili
kuepuka ajari ambazo zinawaacha madereva wengi vilema,”alisema
Mwenisongole, alisema dhamira kuu ya chama chao ni kuhakikisha
madereva wote wa pikipiki wanapata maendeleo katika nyanja kuu mbili ikiwamo
kiuchumi na kijamii na kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika kukuza uchumi
wa taifa na kulipa kodi.
“Changamoto kubwa ni mwitikio wa madereva wengi
kupata mafunzo umekuwa mdogo hii ni kutokana na utamaduni ulio kuwa umejengwa
siku za nyuma madereva kupata leseni bila kupitia mafunzo ya udereva kwenye
chuo kinachotambulika na serikali,”alisema Mwenisongole.
Naye, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Ofisi ya Mkoa wa
Polisi Kinondoni, Samson J. Nguno aliwataka madereva hao kutoendesha bajaji
wakiwa wamelewa ili kupunguza ajari za
mara kwa mara na pia amewataka kuheshimu sheria za barabarani.
Nguno aliwataka madereva hao, kuwafichua waharifu
wanaopora kwani wamekuwa wakitumia vyombo hivyo.
Kwa upande wake, Meneja Masoko wa Kampuni ya
Shinyanga Emporium na wauzaji wa
pikipiki na bajaji aina Piagio, Herman Bernard alisema kampuni hiyo inatoa elimu
ya fursa ya mikopo kwa wajasiriamali na
waendesha Bajaji na Pikipiki.
Herman alisema kuwa bajaji aina ya Piagio inakopeshwa
kwa Sh. Milioni 6.9 ambayo italipwa kwa miezi 18.
Ni vizuri sana nimeipenda ila swali langu ni kwanini hamjanialika? mnikumbuke nami nina jambo ambalo ningeongeanao naomba ikitokea tena mnialije niwasikilize pamoja nakuchangia mada.
ReplyDeleteAhsante.