WENYE SHIDA ZA MAOMBI NA MAOMBEZI WAZIDI KUFUNGULIWA MLIMANI CITY.
Askofu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania (KMUT) Emmaus Bandekile Mwamakula, akimuombea mama huyu aliyesafiri kutoka Morogoro yeye pamoja na mume wake kuja kuombewa Mlimani City Worship Centre (MCC) siku ya jumapili tarehe 16/7/2017.
Familia nzima ilikuwa inaandamwa na magonjwa, binti yao mdogo anayesoma Shule ya Msingi alikuwa anasumbuliwa na pepo la pumu ambalo lilimsababishia kukosa masomo mara kwa mara na pesa nyingi kutumika kwa ajili ya matibabu pasipo kupona.
Pia binti zao wengine wawili walikuwa wakiteswa na nguvu za giza akiwamo mmoja ambaye alikuwa katika hali ya mateso kwa muda wa zaidi ya miaka 10 na baba yao alifikia hatua hata ya kupooza mkono mmoja.
Wazazi walipopata taarifa za maombezi pale Mlimani City waliwatanguliza kwanza watoto wao na walipopata taarifa kuwa watoto wao wamefunguliwa, na walipomuona kwa macho yao binti yao ambaye baada ya kuombewa alirudi Mkoani Morogoro na wazazi hao waliamua kufunga safari kuja Dar es Salaam katika maombi ya awali yaliyofanyika katika makazi ya Askofu.
Pepo lililokuwa likimtesa mwanaume lilimtupa chini kama gunia kisha likamuachia na pepo lililokuwalikimtesa mwanamke lilimtupa chini yule mama na kumuachia, familia ilirudi Morogoro siku ya Jumatatu tarehe 17/7/2017 ikiwa na furaha baada ya kufunguliwa kwa Jina la Yesu.
Ibada za sifa, maombezi na kufunguliwa hufanyika kila Jumapili kuanzia saa 2:00 hadi saa 5:00 asubuhi katika ukumbi wa Sinema uliopo ndani ya Mlimani City, hakuna malipo yeyote wala tozo, watu wanaosumbuliwa na magonjwa na vifungo wanakaribishwa kuja kuombewa bure kwa jina la Yesu.
Ibada hizi pia hufanyika muda huo huo katika vituo vingine kikiwemo cha Kanisa la Moravian la Ushirika wa Uamsho Tanzania, Ushirika wa Golani eneo la Kimara Suka, Usipoteze pesa yako na muda njoo upate uponyaji bure kwa Jina la Yesu, kwa mawasiliano zaidi 0767086884.
Comments
Post a Comment