Posts

BUNDU, MBUNIFI WA SIMU YA "KIFUU"AMBAYE HAKUNUFAIKA NA KAZI YAKE.

Image
Bundu, akiwa na vitu vingine alivyobunia ambavyo ni kobe wakieletroni pamoja na simu yenye umbo la ndege mnyama. Peter Akaro. ALLY Bundu ni kijana ambaye ana jishughulisha na ubunifu kwa kipindi kirefu, ingawa kwasasa amekata tamaa kutokana na mambo aliyokutana nayo katika kazi za ubunifu. Kabla ya hayo, Bundu amebuni Simu ya Mezani ya Kifuu cha Nazi, hii simu ni kwaajili ya kudhibiti upotevu wa simu kadi (hasa kwa kipindi cha nyuma ambapo kulikuwa hakuna huduma ya kurejesha simu kadi). Simu hii ya kifuu inaweza kutumikia wakati haina simukadi (laini), pengine mtumiji ameificha sehemu isiyoweza kuonekana na wezi, na mtumiaji anaweza kuwasiliana bila matatizo yoyote ya kimtandao. Vitu vilivyo unda simu.     Anasema kitu cha kwanza ni kifuu cha nazi kama kava la nje, kandambili kwaajili vibonyezeo (baton), wayaza ‘transformer’, kioo (display) cha simu ya Motorola, kadi ya deki ya runinga (simsung) kwaajili ya kunukuu mtandao (network). “Kadi ni kwaajil...

MWIMBAJI WA INJILI CHRISTINA AKITUMBUUZA KWENYE HAFLA HIYO YA UFUNGUZI WA MABWENI NA HARAMBEE YA KITUO HICHO.

Image
  Mwimbaji wa nyimbo za Injili Christina Mbilinyi akitumbuiza nyimbo kwenye hafla hiyo, iliyofanyika kwenye kituo hicho Bagamoyo Mkoani Pwani.   Christina Mbilinyi akiendelea kutumbuiiza kwenye hafla hiyo leo . Mwimbaji Mbilinyi akiimba kwa hisia, akiwa na baadhi ya wadau walioshiriki kwenye hafla hiyo.( PICHA ZOTE NA MAISHA NI HABARI BLOG).

DIWANI URIO AWA MIONGONI MWA WALEZI WA KITUO CHA WATOTO YATIMA AMANI ORPHANAGE.

Image
  Na Enles Mbegalo DIWANI wa Kata ya Kunduchi jijini Dar es Salaam, Michael Urio,amejitolea kuwa miongoni mwa wazazi watakao kuwa walezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Amani Orphanage, kilichopo Bagamoyo Mkoa wa Pwani. Aidha, Diwani Urio  alijitolea wakati  alipokuwa mgeni rasmi katika uchangishaji wa harambee kwaajili ya kuchangisha fedha za kusaidia katika kutatua baadhi ya changamoto zilizopo kwenye kituo hicho. “Na mimi nitakuwa miongoni mwa wazazi watakao lea kituo hiki na shida yangu itakuwa shida yao, kama nilivyo mzazi wa familia yangu naomba niwe mzazi wa kituo hiki,”alisema Urio na kuongeza kuwa “Mkurugenzi usisite kunishirikisha kitu chochote iwe chakula, mavazi, malazi nitawasaidia kwa nilichonacho na nitawasaidia kuomba kwa wadau mbalimbali kwaajili ya watoto hawa,” Hata hivyo pamoja na ulezi huo Diw ani Urio aliahidi kutoa Sh. Milioni moja pamoja kusaidia kufikisha umeme kwenye eneo hilo kutokana na kutokuwa na umeme. Pia D...

WADAU WAMEOMBWA KUSAIDIA WATOTO YATIMA.

Image
  Na Enles Mbegalo MKURUGENZI wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Amani Orphanage, Magreth  Mwegalawa,kilichopo Bagamoyo Mkoa wa Pwani amewaomba wadau mbalimbali kujitoa  kwa moyo katika kusaidia watoto hao. Hayo aliyasema leo mkoani humo wakati wa ufunguzi wa mabweni mawili ya kulala watoto wa kiume na wakike kwenye kituo hicho. “Kutoa ni moyo nawaomba wadau mbalimbali wajitoe kwaajili ya watoto wasiojiweza kwani kufanya hivyo ni kupata dhawabu kwa Mwenyezi Mungu,”alisema Mwegalawa. Alisema changamoto zilizopo kwenye kituo hicho ni za kawaida ikiwamo kukosa chakula, vifaa vya shule hasa kwa kipindi cha miezi ya kuanza shule na kufungu. Aliongeza kuwa kituo hicho kilianza na watoto wawili ambapo hadi sasa wamefikia watoto 38. Pia alisema kituo hicho kinapokea watoto hao kuanzia kuzaliwa. MKURUGENZI wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Amani Orphanage, Magreth    Mwegalawa,akiwa ameongozana na Mchungaji wa Kanisa la Luthe...

ASILIMIA 10 YA WANAUME WAPO HATARINI KUPATA TEZI DUME .

Image
Na Enles Mbegalo ASILIMIA 10 ya wanaume waliofikia umri wa miaka 40 wapo hatarini kupata ugonjwa wa tezi dume. Akizungumza na mwandishi wa blog hii , Mtaramu wa Madawa na Tiba ( PharmD),  kutoka Hospitali ya Sanitas jijini Dar Es Salaam, Doctar Sajjad Fazel alisema ugonjwa huo nirahisi kuupata kadri umri unavyoongezeka. “Asilimia 10 ya wanaume waliozidi  umri wa miaka 40 na waliozidi miaka 60 wanapata tezi dume na kadri umri unavyoongezeka unapata tezi dume,” alisema na kuongeza “Tenzi dume ni kiungo kinachopatikana chini ya kibofu cha mkojo na kinazunguka milija ya mikojo,” DK. Fazel alisema dalili ya tezi dume ni kukojoa mara kwa mara, kuchukua muda mrefu ukitaka kukojoa,mkojo kutotoka kikamilifu,kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa. Alisema dalili nyingine ni kupata maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa na ikifikia hatua za mwisho za tezi dume inatoka damu kwenye mkojo. “Ugonjwa huu ukitambulika mapema unaweza kutibika kwa kutumia dawa...

VIONGOZI WANAOFICHA MATUKIO YA UKATILI DHIDI YA WATOTO KUCHUKULIWA HATUA.

Na Mwandishi Wetu, Mufindi MKUU wa Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, Jamhuri William amewatahadharisha viongozi na watendaji vijiji na kata kuwa atawachukulia hatua kali za kisheria kutokana na tabia zao za kuficha matukio ya ukatili dhidi ya watoto. Mkuu huyo wa wilaya ametoa onyo hilo mjini Mafinga kwenye mkutano maalumu wa kuainisha mikakati ya kuimarisha ulinzi na usalama wa watoto wilayani humo. Akiongea wakati wa mkutano huo ambao ulizikutanisha   taasisi mbalimbali ikiwamo jeshi la polisi,mahakimu wa mahakama ya wilaya, taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru), jeshi la magereza na uhamiaji pamoja na viongozi wa dini na kimila.  Alisema vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vimefikia hatua ya kutovumilika na hatua zaidi zinapaswa kuchukuliwa ili kukomesha vitendo hivyo. Aliongeza kuwa kwa mwaka huu  katika kipindi  cha miezi mitatu matukio 53 yanayohusu ukatili dhidi ya watoto yameripotiwa na katika kipindi cha mwaka 2013 hadi 20...

WANACHAMA WATATU WA MAZOMBE SACCOS WAFUKUZWA UANACHAMA.

  Na Mwandishi Wetu, Ilula CHAMA   cha ushirika cha akiba na mikopo cha Mazombe Saccos Ltd,kilichopo kwenye mji mdogo wa Ilula wilayani Kilolo mkoani Iringa kimewafukuza wanachama wao watatu akiwamo makamu mwenyekiti wa chama hicho  Ephrem Mgao kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo uchochezi. Aidha,waliosimamishwa  uanachama huo ni Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Ephrem Mgao kwa sababu ya uchochezi,Ezekiel Mkusa na Rehema Myega ambao wote wawili walikuwa wamepoteza sifa za fungamano la chama. Uamuzi huo umekuja mwishoni wa wiki kwenye mkutano mkuu wa 15 wa chama  hicho ambapo Mwenyekiti wa chama hicho, Yohana Mwemutsi alisema kuwa walipata taarifa kutoka kwa wanachama wenye nia njema na chama hicho kwamba kuna mtu anatoa taarifa za uchochezi juu ya chama hicho. “Tulifanya uchunguzi  na tuligundua Mgao ndiye chanzo ,tuliamua kuitisha kikao kikao cha bodi na kumueleza kuwa yeye ndiye chanzo cha uchochezi katika chama na kumueleza sababu z...