JET IMEITAKA SERIKALI KUWARUDISHIA ARDHI WANAKIJIJI WA KILWA.

Kushoto ni Mwanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET), Aisia Rweyemamu, katikati ni Mjumbe wa Bodi ya JET, Leah Mushi na kulia ni Mosses Masenga wakizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, kuhusu ardhi iliyotelekezwa na Muwekezaji katika vijiji vya Mavuji, Migeregere, Nainokwe na Liwiti katika Wilaya ya Kilwa.

Na Mwandishi Wetu.

CHAMA cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET), kimeitaka Serikali kuchukua hatua ya kuwarudishia ardhi wanakijiji wa Wilaya ya Kilwa  iliyochukuliwa na Muwekezaji ili kuondoa umasikini na kujiletea maendeleo.

 Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam, Mjumbe wa Bodi ya  JET, Leah Mushi alisema Muwekezaji huyo alichukua ardhi hiyo  kwa lengo la kuwekeza katika kilimo cha mibono lakini kampuni hiyo haikufanya uwekezaji wowote na badala yake ilijishughurisha na uvunaji wa misitu na utengenezaji wa mbao.

“ Sisi kama Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania  tunaitaka Serikali ichukue hatua ya kuingilia kati na kuwarudishia ardhi wanavijiji wa Mavuji, Migeregere, Nainokwe na Liwiti kwani wanahitaji ardhi hiyo ili kuondoa umasikini na kujiletea maendeleo,”alisema Mushi kuongeza

“Muwekezaji  huyo ametelekeza ardhi kwa muda mrefu hivyo tunaomba irudishwe kwa wananchi kama ambavyo Serikali imefanya kule Morogoro, Kapunga Wilayani Mbarali, Kigamboni na kwingineko,”

Hata hivyo, Serikali ya kijiji  na wananchi wameiomba serikali kuchukua hatua za kisheria ili ardhi hiyo kurudi kwani imetelekezwa kwa muda mrefu na haina manufaa kwa wananchi kama itaendelea kubaki.

“Mahitaji ya ardhi kwa wananchi yameongezeka hasa kwaajili ya kilimo na ufugaji  kwa sasa baadhi ya familia za wakulima hutembea kilometa nane kwa siku ili kwenda shambani na wakati wa masika hulazimika kuhamia huko na hali hii imesababisha baadhi ya watoto kuacha shule,”alisema





Comments

Popular posts from this blog

SERIKALI YAREJESHA KAMBI TANO ZA JKT ZILIZOKUWA ZIMESITISHA MAFUNZO YA JESHI.

BELENG’ANYI, MBUNIFU MWENYE MALENGO YA KUTENGENEZA MGODI WA KUFUA UMEME.

WAKULIMA WA ZAO LA VITUNGUU IRINGA WATELEKEZA MASHAMBA.