Posts

MAOMBEZI YA ALHAMISI YA LEO KATIKA KANISA LA CHRISTIANI LIFE LILILOPO TEGETA NYUKI.

Image
Mchungaji Mkuu wa Kanisa la Christian Life, Eliya Peter akimuombea mmoja wa waumini wa kanisa hilo leo, katika kipindi cha maombezi ambacho hufanyika kila siku ya Alhamisi katika Kanisa hilo lililopo Tegeta Nyuki jirani na Shule ya Sekondari ya CANOSSA  jijini Dar es Salaam. Mchungaji Mkuu wa Kanisa hilo Eliya pamoja na wahudumu wengine wa kanisa hilo wakiendelea kutoa huduma ya maombizi leo katika kanisa hilo. Waumini waliofika leo kwenye kanisa hilo kwaajili ya maombi wakifuatilia watu wanavyofunguka katika maombezi hayo leo jijini Dar es Salaam.   Mchungaji Mkuu wa Kanisa hilo Elia akiwa na wahudumu wengine wa kanisa hilo wakiendelea kutoa huduma leo.  Maombezi yakiendelea leo katika kanisa hilo ambalo hutoa huduma hiyo ya maombi kila siku ya Alhamisi.   Mchungaji Mkuu wa Kanisa hilo, Eliya akiendelea kumwombea mtu mmoja mmoja huku watumishi wa kanisa hilo wakiendelea kutoa huduma kwa watu wanaoombewa. Watumishi wa kanisa...

MAKINDA KUFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA KUJADILI MAENDELEO YA TANZANIA NA KOREA KESHO.

Image
Na Mwandishi Wetu. SPIKA  wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mstaafu Anne Makinda ,  anatarajiwa kufungua mkutano  wa wadau mbalimbali wa kujadili maendeleo ya Tanzania na Korea Kusini na nchi nyingine za Asia kesho jijini Dar es Salaam. Aidha mkutano huo wa siku tatu utafanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Budget Entertainmemt Resort uliopo karibu na Hotel ya Bahari Beach. Akizungumza na mwandishi wa blog hii, Rais na Mwazirishi wa Taasisi  hiyo  isiyokuwa ya Kiserikali ya Chingu Kota Centre, Andrew Dyson Bukuku alisema mkutano huo utajadili maendeleo mbalimbali  ikiwamo kwa nini Korea Kusini imepiga hatua kiuchumi. Bukuku alitolea   mfano wa miaka ya 1970 na 1980 ya nchi ya Korea ilikuwa tofauti kiuchumi  na sasa na nchi hiyo imeweza kupiga hatua kwa maendeleo. Alisema kuwa  miaka hiyo Korea Kusini uchumi wake ulikuwa sawa sawa na nchi za Afrika lakini leo hii nchi hiyo ni moja kati ya nchi zenye uchum...

UTAFITI: 'UGONJWA WA SELIMUNDU UNA UHUSIANO NA MALARIA KALI'

Image
NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM TAFITI mbalimbali zinaoendelea kufanyika zinaonesha ugonjwa  wa selimundu unaonekana kuwapo kwa kiwango kikubwa katika sehemu zenye malaria kali ikilinganishwa na maeneo mengine, imeelezwa. Mratibu wa Mradi wa Kuelimisha Jamii kuhusu ugonjwa wa selimundu nchini (PPE), Promise Mwakale alisema hayo mwishoni mwa wiki alipozungumza na MTANZANIA kwenye viwanja vya Mbagala Zakheim. “Watafiti wanafikiria kwamba sickcell ina wiana na malaria kali, hata ukiangalia ramani ya dunia inaonesha wazi sehemu zenye malaria kali ndizo zenye tatizo,” alisema.   Alisema watafiti wanafikiri kwamba ugonjwa wa selimundu hulianza kama njia ya mwili kupambana na malaria. “Kwamba ikiwa seli za damu haziwezi kuishi muda mrefu basi hata wale wadudu wa malaria hawawezi kuishi muda mrefu,” alisema. Alisema katika Idara ya sickcell, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wamekuwa wakipokea wagonjwa wengi kutoka Zanzibar, Pwani, Bagamoyo, Mwanz...

UJENZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA OFISI YA TAIFA YA TAKWI MKOANI DODOMA UNAENDELEA.

Image
 Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ikikagua ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya ofisi hiyo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya  ujenzi wa jengo hilo iliyofanyika hivi karibuni  mkoani Dodoma. Ujezi wa jengo hilo unatarajia kumalizika mwanzoni mwa mwaka 2018.   Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ikikagua ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya ofisi hiyo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya   ujenzi wa jengo hilo iliyofanyika hivi karibuni   mkoani Dodoma. Ujezi wa jengo hilo unatarajia kumalizika mwanzoni mwa mwaka 2018.    Taswira ya ujenzi wa   jengo la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS),  mkoani Dodoma. Ujezi wa jengo hilo unatarajia kumalizika mwanzoni mwa mwaka 2018. Taswira ya ujenzi wa   jengo la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)  mkoani Dodoma. Ujezi wa jengo hilo unatarajia kumalizika mwanzoni mwa mwaka 2018. (PICHA ZOTE NA OFISI YA NBS).

MATUKIO YA IBAADA YA LEO, KATIKA KITUO CHA IBAADA CHA MLIMANI WORSHIP CENTRE (MCC).

Image
  ASKOFU     Mkuu wa Dayosisi Kuu ya Dar es Salaam na Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania (KMUT), Emmaus Mwamakula, akimusimika Shemasi Mlei Neema Mwaipopo  aliyepiga magoti katika kituo cha   Ibada cha Mliman City Worship Centre (MCC), leo.  Picha ya pamoja baada ya kusimikwa kwa Mlei Neema, wa pili kutoka kushoto.   Askofu Mwamakula akimtambulisha Mwinjilisti Martini Kajituel  akiwa na mke wake leo, walioshiriki ibaada ya leo  katika kituo cha MCC. Askofu Mwamakula akiwa amepiga magoti kwenye picha ya pamoja na baadhi ya  watoto waliofika kuabudu leo kwenye kituo cha ibaada cha MCC.   Mwinjilisti Martini Kajituel akitoa mahubili leo katika kituo cha ibaada  cha MCC,  na somo la leo limetoka katika kitabu cha Luka 8: 43-48.  Waumini wakiendelea kusifu katika kipindi cha Sifa  leo, katika kituo cha ibaada cha MCC.   Waumini wakiendelea kusifu na kuabud...

MWENYEKITI MUNENI ATEMBELEA MAENEO ALIYOTOA AGIZO YABORESHWE NA KUTENGENEZWA BUSTANI ZA MAUA.

Image
  Muneni akimuonyesha Afisa Utawala wa Kanisa la Mtakatifu Albani, Danny Malonga maeneo ambayo wanatakiwa kuyaboresha na kutengeneza busatani na kutengeneza taa. Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Sea View, Kata ya Kivukoni, Victor Muneni, kushoto  akizungumza na Afisa Utawala wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Albano(Anglikana), Danny Malonga leo,  wakati alipomtembelea ofisini kwake kwaajili ya kuzungumzia uboreshaji wa mazingira ya maeneo yanayowazunguka kwaajili ya kutengeneza bustani na kupanda maua. Mwenyekiti Muneni akionyesha bango la Kampuni ya Puma ambalo limejengwa ndani ya hifadhi ya barabara na amefanya   mazungumzo wa uongozi wa kampuni hiyo,  umeafiki kulifanyia marekebisho bango hilo, ambalo lilikuwa liki sababisha likihatarisha ajali na kuhatarisha watumiaji wa barabara kuwa katika hali hatarishi. Mwenyekiti akionyesha eneo hilo lilikuwa kichaka ambacho kilikuwa kimbilio kubwa la vibaka wanaotoka kwenye fukwe za baharini na ...