WENYE SHIDA ZA MAOMBI NA MAOMBEZI WAZIDI KUFUNGULIWA MLIMANI CITY.
Askofu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania (KMUT) Emmaus Bandekile Mwamakula, akimuombea mama huyu aliyesafiri kutoka Morogoro yeye pamoja na mume wake kuja kuombewa Mlimani City Worship Centre (MCC) siku ya jumapili tarehe 16/7/2017. Familia nzima ilikuwa inaandamwa na magonjwa, binti yao mdogo anayesoma Shule ya Msingi alikuwa anasumbuliwa na pepo la pumu ambalo lilimsababishia kukosa masomo mara kwa mara na pesa nyingi kutumika kwa ajili ya matibabu pasipo kupona. Pia binti zao wengine wawili walikuwa wakiteswa na nguvu za giza akiwamo mmoja ambaye alikuwa katika hali ya mateso kwa muda wa zaidi ya miaka 10 na baba yao alifikia hatua hata ya kupooza mkono mmoja. Wazazi walipopata taarifa za maombezi pale Mlimani City waliwatanguliza kwanza watoto wao na walipopata taarifa kuwa watoto wao wamefunguliwa, na walipomuona kwa macho yao binti yao ambaye baada ya kuombewa alirudi Mkoani Morogoro na wazazi hao waliamua kufunga safari ku...