Posts

JET IMEITAKA SERIKALI KUWARUDISHIA ARDHI WANAKIJIJI WA KILWA.

Image
Kushoto ni Mwanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET), Aisia Rweyemamu, katikati ni Mjumbe wa Bodi ya JET, Leah Mushi na kulia ni Mosses Masenga wakizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, kuhusu ardhi iliyotelekezwa na Muwekezaji katika vijiji vya  Mavuji, Migeregere, Nainokwe na Liwiti  katika Wilaya ya Kilwa. Na Mwandishi Wetu. CHAMA cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET), kimeitaka Serikali kuchukua hatua ya kuwarudishia ardhi wanakijiji wa Wilaya ya Kilwa   iliyochukuliwa na Muwekezaji ili kuondoa umasikini na kujiletea maendeleo.  Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam, Mjumbe wa Bodi ya  JET, Leah Mushi alisema Muwekezaji huyo alichukua ardhi hiyo  kwa lengo la kuwekeza katika kilimo cha mibono lakini kampuni hiyo haikufanya uwekezaji wowote na badala yake ilijishughurisha na uvunaji wa misitu na utengenezaji wa mbao. “ Sisi kama Chama cha Waandishi wa...

WENYE SHIDA ZA MAOMBI NA MAOMBEZI WAZIDI KUFUNGULIWA MLIMANI CITY.

Image
Askofu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania (KMUT) Emmaus Bandekile Mwamakula, akimuombea  mama huyu aliyesafiri kutoka Morogoro yeye pamoja na mume wake kuja kuombewa Mlimani City Worship Centre (MCC) siku ya jumapili tarehe 16/7/2017. Familia nzima ilikuwa inaandamwa na magonjwa, binti yao mdogo anayesoma Shule ya Msingi alikuwa anasumbuliwa na pepo la pumu ambalo lilimsababishia kukosa masomo mara kwa mara na pesa nyingi kutumika kwa ajili ya matibabu pasipo kupona. Pia binti zao wengine wawili walikuwa wakiteswa na nguvu za giza akiwamo mmoja ambaye alikuwa katika hali ya mateso kwa muda  wa zaidi ya miaka 10 na baba  yao alifikia hatua hata ya kupooza mkono mmoja. Wazazi walipopata taarifa za maombezi pale Mlimani City waliwatanguliza kwanza  watoto wao na walipopata taarifa kuwa watoto wao wamefunguliwa,  na walipomuona kwa macho yao binti yao ambaye baada ya kuombewa alirudi Mkoani Morogoro na  wazazi hao waliamua kufunga safari ku...

ZOEZI LA KUORODHESHA KAYA KWA AJILI YA UTAFITI WA MAPATO NA MATUMIZI LINAENDELEA KUFANYIKA NCHINI

Image
  Mdadisi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akihoji taarifa za kaya wakati wa zoezi la kuorodhesha kaya kwa ajili ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 linaloendelea kufanyika nchini ikiwa ni maandalizi ya utafiti huo unaotarajia kufanyika hivi karibuni. Mdadisi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akihoji taarifa za kaya wakati wa zoezi la kuorodhesha kaya kwa ajili ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 linaloendelea kufanyika nchini ikiwa ni maandalizi ya utafiti huo unaotarajia kufanyika hivi karibuni. Mdadisi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akiwaoneyesha wasimamizi namna alivyojaza taarifa za kaya wakati wa zoezi la kuorodhesha kaya kwa ajili ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 linaloendelea kufanyika nchini ikiwa ni maandalizi ya utafiti huo unaotarajia kufanyika hivi karibuni.  (PICHA ZOTE NA EMMANUEL GHULA). ...

CHAMA CHA MADEREVA “BAJAJI” KIMEIOMBA SERIKALI KUTOTOA LESENI KWA MADEREVA WASIO NA SIFA.

Image
Mwenyekiti wa chama cha Maendeleo ya Madereva Pikipiki Matairi Matatu Tanzania, Edward Mwenisongole akizungumza na madereva hao leo baada ya mgeni rasmi  Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Ofisi ya Mkoa wa Polisi Kinondoni, Samson J. Nguno, kuwasili katika mkutano huo.   Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Ofisi ya Mkoa wa Polisi Kinondoni, Samson J. Nguno, akisaini kitabu cha wageni baada ya kufika.   Wageni kutoka  Kampuni ya Shinyanga Emporium  na wauzaji wa pikipiki na bajaji aina Piagio, waliofika kwenye mkutano huo leo jijini Dar es Salaam kwaajili ya kutoa elimu ya fursa juu ya mikopo ya bajaji na pikipiki.  Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Ofisi ya Mkoa wa Polisi Kinondoni, Samson J. Nguno, akimkabidhi cheti  mmoja wa madereva wa bajaji waliohitimu mafunzo hayo ya wiki mbili na kutunukiwa vyeti leo.    Madereva wa bajaji waliotunukiwa vyeti leo wakinyoosha mikono baada ya Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Ofisi ya Mkoa wa Poli...

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA KWA MWEZI JUNI, 2017 UMEPUNGUA.

Image
  Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephraim Kwesigabo (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza Mfumuko wa Bei wa Taifa wa mwezi Juni, 2017 ambao umepungua hadi asilimia 5.4 kutoka asilimia 6.1 mwezi Mei, 2017. Kushoto kwake ni Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira, Ruth Minja. Baadhi ya Waandishi wa habari waliohudhuria katika Mkutano wa kutangaza Mfumuko wa Bei wa Taifa wa mwezi Juni, 2017 uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Mfumuko wa bei umeonyesha kupungua hadi asilimia 5.4 kutoka asilimia 6.1 mwezi Mei, 2017.  ( PICHA NA EMMANUEL GHULA) Na,Veronica Kazimoto. MFUMUKO wa Bei wa Taifa kwa mwezi Juni, 2017 umepungua hadi asilimia 5.4 ikilinganishwa na asilimia 6.1 ilivyokuwa mwezi Mei, 2017. Akizungumza na waandishi wa Habari jana jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephraim Kwesigabo amesema ...

ZOEZI LA KUOROZESHA KAYA KWA AJILI YA UTAFITI WA MAPATO NA MATUMIZI KUANZA LEO

Image
Meneja wa Takwimu za Jamii na Watu Bi. Sylvia Meku akizungumza wakati wa mafunzo ya Wadadisi watakaokwenda kuorozesha kaya mikoa yote kwa ajili ya maandalizi ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18. Zoezi hilo la uorozeshaji kaya litafanyika kwa muda wa siku kumi na tano (15) kuanza leo  Julai 11, 2017.  Baadhi ya Wadadisi wakimsikiliza kwa makini Meneja wa Takwimu za Jamii na Watu Bi. Sylvia Meku (hayupo Pichani) wakati wa mafunzo ya Wadadisi watakaokwenda kuorozesha kaya mikoa yote kwa ajili ya maandalizi ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18. Zoezi hilo la uorozeshaji kaya litafanyika kwa muda wa siku kumi na tano (15) kuanza leo Julai 11, 2017.  Baadhi ya Wadadisi wakiwa kwenye gari wakielekea Kata ya Mchikichini, Ilala na Kawe jijini Dar es Salaam kufanya mazoezi ya kuorozesha kaya kwa vitendo kwa ajili ya maandalizi ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzan...

SOMA MAGAZETI YA JUMAMOSI LEO, JULAI 8,2017.

Image