Posts

Showing posts from September, 2017

JET IMEITAKA SERIKALI KUWARUDISHIA ARDHI WANAKIJIJI WA KILWA.

Image
Kushoto ni Mwanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET), Aisia Rweyemamu, katikati ni Mjumbe wa Bodi ya JET, Leah Mushi na kulia ni Mosses Masenga wakizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, kuhusu ardhi iliyotelekezwa na Muwekezaji katika vijiji vya  Mavuji, Migeregere, Nainokwe na Liwiti  katika Wilaya ya Kilwa. Na Mwandishi Wetu. CHAMA cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET), kimeitaka Serikali kuchukua hatua ya kuwarudishia ardhi wanakijiji wa Wilaya ya Kilwa   iliyochukuliwa na Muwekezaji ili kuondoa umasikini na kujiletea maendeleo.  Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam, Mjumbe wa Bodi ya  JET, Leah Mushi alisema Muwekezaji huyo alichukua ardhi hiyo  kwa lengo la kuwekeza katika kilimo cha mibono lakini kampuni hiyo haikufanya uwekezaji wowote na badala yake ilijishughurisha na uvunaji wa misitu na utengenezaji wa mbao. “ Sisi kama Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania