Na Enles Mbegalo UONGOZI wa Soko la Samaki Kunduchi, Dar es Salaam limeunda Kikundi cha Ulinzi Shirikishi cha Pwani na Baharini (BMU), kwa lengo la kudhibiti uvumi haramu. Akizungumza na mwandishi wa blog hii, mmoja wa viongozi wa soko hilo, Ramadhani Ali, alisema kikundi hicho cha watu 15 kitafanya doria kwenye fukwe za bahari kwa masaa 24 ili kuwadhibiti wavuvi hao pamoja na wachafunzi wa mazingira ya fukwe hizo. “Ulinzi huu wa baharini utasaidia sana kuwaokoa baadhi ya samaki ambao wameaza kupotea kabisa baharini na tutagundua ni samaki wapi hawapatikani kwa sasa na kipindi cha nyuma walikuwa wanapatikana,”alisema Ali Pia, alisema pamoja na serikali kupiga vita uvuvi huo ila inatakiwa kuwasaidia wavuvi hao vifaa vya kisasa kwaajili ya kuvitumia katika shughuri zao za uvuvi. Hata hivyo, alisema soko hilo limekuwa likikabiliwa na changamoto mbalimba ikiwamo usalama mdogo kwa wavuvi kwani wamekuwa wakitishiwa maisha yao na vij...
Comments
Post a Comment